Ebola yaripotiwa Mbale, Mashariki ya Uganda

  • | KBC Video
    2 views

    Wizara ya afya iko katika tahadhari kuu kufuatia kuripotiwa kwa kisa cha ugonjwa wa Ebola mjini Mbale, mashariki ya Uganda, ulio chini ya umbali wa kilomita-70 kutoka eneo la mpakani la Malaba. Mikakati hiyo inajumuisha kuimarishwa kwa uchunguzi katika viingilio vya humu nchini huku maegesho maalum yakitengwa kwa ndege zinazowasili kutoka nchini Uganda. Wananchi wamehimizwa wawe waangalifu zaidi huku serikali ikishauriana na halmashauri ya kusambaza vifaa vya matibabu hapa nchini-KEMSA ili kununua dawa za kutosha vikiwemo vifaa vya kujikinga katika juhudi za kujiandaa kwa hali yoyote inayoweza kutokea. Kufikia leo, Uganda imethibitisha visa-9 vya maradhi ya Ebola.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive