Familia yamtaka Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Masengeli kusema aliko mwakilishi wadi wa Della

  • | Citizen TV
    1,149 views

    Familia ya mwakilishi wadi wa Della kaunti ya Wajir, Yusuf Hussein Ahmed aliyetoweka Ijumaa iliyopita, sasa imemfungulia mashtaka inspekta jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli, kutaka aeleze aliko mwakilishi wadi huyo, anayedaiwa kutekwa nyara ijumaa iliyopita. Haya yanajiri huku wabunge wa eneo la kaskazini pia wakitaka serikali kuwajibika na kuhakikisha kuwa mjumbe huyo anafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ikiwa alifanya kosa lolote. Mwakilishi huyo alitoweka ijumaa iliyopita katika mtaa wa South B hapa Nairobi.