Familia Yataka Haki Baada ya Mpendwa Kufukiwa na Kifusi Mombasa

  • | K24 Video
    4,480 views

    Familia ya Yusuf Ali Abdhi, ambaye anadaiwa kufukiwa na kifusi wakati jumba la orofa lilianguka katika eneo la Kona ya Kilifi mjini Mombasa, inaitaka serikali kuharakisha shughuli ya kutafuta mwili wake.Wakizungumza kwa uchungu, jamaa wa marehemu wameomba haki itendeke na uchunguzi wa haraka kufanyika. Wakati huo huo, Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amewasimamisha kazi maafisa wawili kutoka idara ya ujenzi na ardhi ili kutoa nafasi kwa uchunguzi huru kuhusu sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.