Hali ya utulivu mjini Damascus baada ya kupinduliwa Rais wa zamani Assad

  • | VOA Swahili
    355 views
    Video zilizorekodiwa na ndege zisizokuwa na rubani katika mji mkuu wa Syria, Damascus, zinaonyesha kwamba shughuli zinaendelea kama kawaida. Benki zimefunguliwa kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar al-assad, ikiwa ni hatua inayoashiria kurejea kwa hali ya kawaida nchini humo. Video pia zinaonyesha maduka yakiwa yamefunguliwa, sawa na shughuli za ujenzi kuendelea. Usafi pia unaendelea mjini. Hatua ya kupinduliwa kwa utawala wa Bashar imepelekea nchi kadhaa katika eneo hilo na nchi zenye ushawishi mkubwa duniani kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya baadaye ya Syria baada ya waasi kuchukua udhibithi wa nchi. Wakazi wa Damascus wameonekana wakifanya usafi huku wengine wakipiga picha karibu na gari la kijeshi, siku chache baada ya waasi kuudhibiti mji huo. Wakazi wameelezea matumaini kwamba maisha yao yanakuwa sawa baada ya kuanguka kwa utawala wa rais Bashar al-Assad. Baadhi yao wameonekana wakikanyaga picha ya rais aliyepinduliwa na kuyasifu mataifa yote ya kiarabu kwa ushindi huo. Waziri mkuu wa Assad, Mohammed Jalali, amekubali kuachia madaraka kwa waasi. - Reuters #syria #damascus #alassad #voa