Skip to main content
Skip to main content

Idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao kutimia yaongezeka

  • | KBC Video
    15 views
    Duration: 4:39
    Maafisa wa afya wanaonya kwamba taifa hili linakabiliwa na ongezeko la watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wao kuwadia, hii ikiwa mojawapo ya sababu kuu za vifo vya watoto wachanga humu nchini. Kulingana na utafiti wa idadi ya watu na afya wa mwaka 2022, watoto 21 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai huaga dunia, hii ikiwa ni asilimia 51 ya vifo vyote vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Serikali inasema inazidisha bidii katika kupunguza vifo hivyo kwa kuimarisha huduma za utunzi wa watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao kuwadia, kuboresha lishe ya waja wazito, kuongeza idadi ya kina mama wajawazito wanaopata huduma za afya na kuhakikisha kina mama wengi zaidi wanajifungua kwa usaidizi wa wahudumu wa afya wenye ujuzi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive