Idara ya mahakama yataka asasi zote za usalama kuheshimu sheria na kukomesha visa vya utekaji nyara

  • | Citizen TV
    3,337 views

    Idara ya mahakama sasa inataka asasi zote za usalama kuheshimu sheria na kukomesha mara moja, visa vya utekaji nyara ambavyo vimeendelea kushuhudiwa nchini. Taarifa ya idara ya mahakama imejiri huku Tume ya kitaifa ya haki kwa binadamu nchini ikichapisha majina ya watu 7 waliotekwa nyara kwa wiki moja iliyopita ikisema visa 82 vya utekaji nyara vimeripotiwa tangu mwezi juni mwaka huu. Na kama anavyoarifu Emmanuel Too, wakenya kwenye mitandao ya kijamii pia wameonyesha ghadhabu yao kuhusu kutekwa nyara kwa vijana