- 357 viewsDuration: 2:29Tume ya uchaguzi nchini IEBC imewataka wagombea kiti cha ubunge eneo la Kasipul kuandikisha taarifa kuhusu ghasia zilizoshuhudiwa katika eneo hilo wiki hii ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Akizungumza katika makao makuu ya tume hiyo hapa Nairobi, mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon ameonya kuwa huenda baadhi ya wagombea wakaondolewa kwenye uchaguzi wa Novemba 27 ikiwa watapatikana na hatia ya kuchochea vurugu