Tume ya uchaguzi na mipaka humu nchini-IEBC imejitolea kuhakikisha chaguzi ndogo zilizo huru, sawa, wazi na zinazodumisha amani katika maeneo-24 ambako utaandaliwa tarehe 27, mwezi huu.
Akiongea jijini Nairobi, mwenyekiti wa tume ya IEBC Erustus Ethokon aliwahimiza wale wanaoshiriki katika chaguzi hizo kuzingatia maadili, akisema tume hiyo haitaridhia vitendo vyovyote vya uvunjaji sheria. Chaguzi hizo zitakuwa za kwanza kusimamiwa na makamishna wapya wa tume ya IEBC waliochukua hatamu za uongozi mnamo tarehe 11, mwezi Julai mwaka huu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive