Janet Wanja azikwa katika hafla ya maziko ambayo yalikuwa ya kibinafsi Lang'ata jijini Nairobi

  • | Citizen TV
    541 views

    Huzuni na majonzi zilitanda katika eneo la makaburi ya Lang'ata jijini Nairobi wakati ndugu, jamaa, marafiki na wachezaji walipohudhuria mazishi ya mchezaji maarufu wa voliboli Janet Wanja

    Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya voliboli na aliyeheshimiwa ndani na nje ya nchi, alifariki akiwa na umri wa miaka 40, baada ya mapambano na saratani. Familia pamoja na wapenzi wa voliboli wamesimulia jinsi watakavyomkosa hususan alivyojitolea kupigania mafanikio ya mchezo huo nchini.