Je, Ukraine itapona baada ya kuungwa mkono na Ulaya?

  • | BBC Swahili
    366 views
    Baada ya siku kadhaa zilizojaa mihemko ambapo uhusiano kati ya Marekani na Ukraine ulitikisika kutokana na majibizano ya viongozi wa mataifa hayo, Rais Volodymr Zelensky amesema kwamba anahitaji hakikisho la usalama kama jambo muhimu. Amesema pia kwamba Ukraine inahitaji amani, na sio vita visivyokuwa na kikomo. Haya yanajiri baada ya viongozi kutoka bara Ulaya kukutana na kumuunga mkono Rais Zelensky katika kongamano maalum kuhusu vita vya Ukraine na kuhusu mbinu za kusitisha vita dhidi ya Urusi.