Joho afungua soko kubwa la dhahabu mtaani Eastleigh

  • | KBC Video
    514 views

    Waziri wa madini na uchumi wa baharini Hassan Joho amesema dhahabu inayochimbwa humu nchini haitauzwa tena ikiwa ghafi kwa soko la kimataifa. Akizungumza alipofungua soko kubwa la dhahabu mtaani Eastleigh, katika kaunti ya Nairobi, Joho aliwataka wafanyabiashara wa dhahabu hususan kutoka eneo la Kaskazini Mashariki kutuma maombi ya leseni za uchimbaji madini ili kuchunguza na kuchimba madini yaliyogunduliwa hivi majuzi katika eneo hilo. Jamii ya wafanyabiashara katika mtaa huo wa Eastleigh iliitaka serikali kuangazia upya ushuru unaotozwa kwa utengenezaji wa dhahabu ili kukuza soko la dhahabu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive