Kampuni ya Lucid Dream Ltd inasisitiza umuhimu wa wanunuzi wa nje

  • | VOA Swahili
    191 views
    Upendo Kibona, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lucid Dream Limited, anasema kuwa madini ya Tanzania yanapouzwa ndani pekee, thamani yake inabaki kuwa ndogo. Alisisitiza kuwa ni muhimu wanunuzi wa kimataifa washiriki moja kwa moja kwenye minada nchini. "Tunaogombania haya madini ni Watanzania sisi wenyewe. Wale watu wa nchi za nje wakija hapa Tanzania kuyanunua haya madini, ndio pale tutapata masoko ya kuyauza nje ya nchi. Lakini yanaponunuliwa kwa Watanzania wenyewe, inakuwa ni ngumu kuwa na thamani kubwa," alisema Kibona. Wanunuzi wanasema kuwa kuanzishwa kwa mnada huo wa kidijitali utasaidia kurudisha na kuongeza thamani ya madini nchini kwa kuimarisha ushindani sokoni na hivyo kusaidia wanunuzi hao kupata bei nzuri. Ripoti ya Amri Ramadhani, VOA, Tanzania. #tanzania #mfumo #kidigitali #madini #ununuzi #uuzaji #sokolabidhaa #nicholauskaserwa #mererani #manyara #mkoa #voa #voaswahili #luciddreamltd