Kaunti ya Nairobi yarundika taka nje ya jengo la Kenya Power

  • | KBC Video
    2,567 views

    Kizaazaa kilizuka katika makao makuu ya kampuni ya umeme, Kenya Power la Stima Plaza jijini Nairobi, baada ya wafanyakazi wa serikali ya kaunti ya Nairobi kurundika takataka nje ya jengo hilo na kuyabana magari kutokana na mzozo kuhusu bili za umeme. Serikali ya kaunti ya Nairobi imekuwa ikilumbana na kampuni hiyo ya usambazaji umeme kuhusu mzozo wa shilingi bilioni 3. Serikali ya kaunti inaishutumu kampuni hiyo kwa kukatiza umeme mara kwa mara na kukataa kulipa ada za ardhi inayotumiwa kwa shughuli za kusambaza umeme. Kwa upande wake Kenya Power inasisitiza kuwa lazima serikali ya kaunti ilipe bili zote za umeme zilizosalia ili kuepuka kukatiwa umeme.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News