Kenya na Uingereza zimeafikiana kuimarisha mahusiano ya kidiploasia na maendeleo baina yao. Akiongea jijini Nairobi wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Mfalme Charles III,Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi alisema serikali ya Kenya itaendelea kuimarisha maadili yanayoainisha ushirikiano wake na Uingereza. Alitaja mkakati baina ya Kenya na Uingereza uliotiwa sahihi mwezi Julai mwaka huu ambao unatoa mwongozo wa ushirikiano katika nyanja za biashara, uwekezaji, mabadiliko ya tabianchi, ulinzi, sayansi na teknolojia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive