Kesi dhidi ya mhubiri tata Paul Mackenzie yaendelea mahakama ya Mombasa

  • | Citizen TV
    703 views

    Makahama ya Mombasa imeanza kusikiza kesi inayomkabili mhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wengine 94. Mshukiwa wa kwanza amekamilisha kutoa ushahidi na kuelelezea jinsi mackenzie alivyohusika na mauwaji ya watu 238 msituni shakahola kaunti ya Kilifi. Mshukiwa huyo aliiambia mahakama kuwa mackenzie na washukiwa wengine walitumia dini kuwapotosha watu na kisha kuwauwa msituni humo. Hata hivyo wakili wa washukiwa amepuuza madai akisema taarifa hiyo ni njama dhidi ya mackenzie na wenzake walioko kizimbani. Kesi itaendelea hapo kesho.