Kiongozi wa chama tawala akubali kushindwa, upinzani furahani

  • | VOA Swahili
    125 views
    Uchaguzi Ghana: Wafuasi wa Upinzani washerehekea ushindi baada ya makamu wa rais kukubali kushindwa Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Ghana walisherehekea nje ya ofisi ya makao makuu ya chama chao siku ya Jumapili, baada ya Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia kukubali kushindwa na rais wa zamani, John Mahama, siku moja baada ya uchaguzi. Mgombea wa Chama cha National Democratic Congress alithibitisha ushindi wake kupitia mtandao wa X, ambao ulikuwa ukijulikana kama Twitter, kama “ushindi wa wazi.” Makamu wa rais wa Chama tawala cha New Patriotic Party alimpigia simu kumpongeza, Mahama alisema. Tume ya Uchaguzi bado haijatangaza matokeo rasmi. #ghana #uchaguzi #habari #afrika #voaafrika