Kiongozi wa walio wengi asisitiza hoja ya kumbandua naibu rais itapitishwa seneti

  • | KBC Video
    827 views

    Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa amesisitiza kuwa hoja ya kumbandua naibu rais Rigathi Gachagua itapitishwa katika bunge la seneti baada ya wabunge 282 wa bunge la kitaifa kuunga mkono hoja sawia na kuidhinisha kuondolewa kwake mamlakani. Akiongea wakati wa hafla ya kuwakabidhi wanafunzi hundi za fedha za kufadhili masomo, Ichung’wa alisema kuwa bunge sasa linasubiri kwa hamu na ghamu kuona nani atakayeteuliwa kumrithi Gachagua. Mbunge huyo wa eneobunge la Kikuyu alisema kuwa bunge la kitaifa litamsaili atakayeteuliwa kabla ya kumuapishwa rasmi kuwa naibu wa rais

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive