- 2,599 viewsDuration: 2:07Maaskofu wa kanisa katoliki wameonya kuwa huenda sheria mpya ya kudhibiti mitandao ikatumiwa kuwazima wanaopinga serikali na kuhujumu haki za kimsingi za wakenya. Kwenye kikao na wanahabari, maaskofu hao wamesema kuwa kuna haja ya sheria hiyo kuangaziwa upya na vipengee vya ukandamizaji kuondolewa. Maaskofu wanasema kuwa sheria hiyo ilipitishwa kwa haraka na bila umakini. Hata hivyo wamewarai wakenya kudumisha nidhamu mitandaoni