Machifu 5 waliotekwa nyara Mandera waachiliwa Somalia

  • | Citizen TV
    816 views

    Machifu watano waliotekwa nyara na wanamgambo wa Alshabab mapema mwezi Februari kaunti ya Mandera wamewachiliwa huru. Kuachiliwa kwao kumefuatia majadiliano ya takriban miezi miwili. Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen akisema watano hao waliachiliwa na kupokezwa serkali ya Kenya na watawasili nchini wakati wowote.