Mamia ya wakenya hii leo walijipata kwenye njia panda baada ya mtandoa wa e -Citizen kukwama.

  • | Citizen TV
    9,796 views

    Wengi wa walioathirika ni watalii ambao ziara zao zilicheleweshwa huku maafisa wanaosimamia shughuli katika hifadhi za wanyama pori wakilazimika kutafuta njia mbadala ya kupokea malipo

    Katika taarifa yake, mkurugenze mkuu wa mtandao wa e-Citizen Isaac ochieng alisema hitilafu hizo zilitokana na hitiliafu za kimitambo ambazo ziliathiri mtandao huo. Hata hivyo ameomba radhi na kuwahakikishia wakenya kwamba shughuli zimerejeshwa. Wakenya kwa upande wao wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ili kuhakikisha kwamba shughuli hazitatiziki