Marekani yataka madini ili kuisaidia DRC kupamba na M23

  • | BBC Swahili
    3,356 views
    Waasi wa M23 huko DRC wanaendelea kuteka maeneo zaidi mashariki mwa taifa hilo na kukaribia eneo jingine lenye utajiri wa madini. Haya yanajiri huku kukiwa na ripoti kwamba Marekani inafanya mazungumzo na serikali ya DRC kuhusu kuipa DRC msaada wa kijeshi na kisha Marekani kupata fursa ya kuchimba madini muhimu kutoka nchini humo. Nchi hiyo ina utajiri wa madini mengi kama kobalti, lithium, dhahabu na uranium na inaonekana hii inaweza kuvutia utawala mpya wa Trump ambao unaripotiwa kuwa wazi kufanya makubaliano, sawa na yale yanayopendekezwa kwa taifa la Ukraine.