Mashirika ya KBC na Xinhua yadhamiria kushirikiana

  • | KBC Video
    6 views

    Shirika la utangazaji humu nchini-KBC na lile la habari la China, Xinhua yametia saini mkataba wa maelewano utakaofanikisha ubia baina yao katika nyanja mbalimbali. Mkurugenzi mkuu wa shirika hili Agnes Kalekye amesema KBC inanuia kuimarisha sekta tatu muhimu kupitia usaidizi wa shirika la habari la Xinhua ikiwemo kuboreshwa kwa vifaa vya kupeperusha matangazo, mafunzo ya kiteknolojia na ustawishaji wa mfumo wake wa kidijitali. Kalekye aliyasema hayo alipopokea ujumbe maalum kutoka shirika hilo ukiongozwa na makamu wa rais wa shirika hilo duniani Yuan Bingzhong ambao walizuru makao makuu ya shirika la utangazaji la KBC.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive