Skip to main content
Skip to main content

Matunda ya mfenesi yatumiwa kutengeneza divai Busia

  • | Citizen TV
    1,405 views
    Duration: 4:34
    Wakulima katika kaunti ya Busia na eneo pana la magharibi wamehimizwa kukumbatia upanzi wa mmea uliopuuzwa wa fenesi, baada ya wanafunzi wa chuo cha kifundi cha Dr. Daniel Wako Murende kuanzisha shughuli ya kusindika divai kutoka kwa matunda hayo. Ni shughuli iliyoanzishwa mwaka mmoja uliopita, uvumbuzi huo ukipokelewa vema ikizingatiwa kuwa hapo awali, matunda ya mfenesi ambao huzaa nyakati zote za mwaka yalitupwa kiholela na hata kulishwa mifugo.