Mawaziri Geoffrey Ruku, Hanna Cheptumo na makatibu 14 wameapishwa

  • | Citizen TV
    224 views

    Mawaziri Geoffrey Ruku na Hanna Cheptumo ni miongoni mwa maafisa wakuu 16 ambao wameapishwa rasmi hii leo kuanza kutekeleza majukumu yao . Geoffrey Ruku sasa ndiye waziri wa utumishi wa Umma na Hanna Cheptumo ni waziri wa Jinsia. Jumla ya Makatibu 14 vile vile wameapishwa rasmi wakiwemo Stephen Isaboke ambaye bunge lilimuidhinisha lakini kutoa wito kwa rais kumbadilishia wizara kutokana na uhusiano wake na kampuni ya GOTV. rais william ruto ameelezea imani yake kuwa Mawaziri na makatibu wapya watatekeleza majukumu yao ipasavyo.