Mazishi ya mtoto wa miaka 12 aliyeuwawa Ukingo wa Magharibi, Mpalestina ajisalimisha

  • | VOA Swahili
    284 views
    Wananchi wa Israeli walifanya mazishi mjini Jerusalem ya mtoto wa miaka 12 Yehoshua Aharon Tuvia Simha, ambaye aliuwawa katika shambulizi la bunduki kwenye basi katika eneo linalokaliwa kimabavu huko Ukingo wa Magharibi siku ya Alhamisi Shambulizi hilo lilitokea kati ya saa sita usiku Jumatano na mapema Alhamisi, na watu wasiopungua wanne walijeruhiwa. Jeshi la Israeli lilisema kuwa katika kumfuatilia mtu huyo aliyefanya shambulio hilo, Mpalestina huyo alijisalimisha kwa vyombo vya usalama. Ghasia huko Ukingo wa Magharibi tayari ziliongezeka kabla ya vita vya Gaza kuanza Oktoba 7 mwaka jana na zimeendelea kuongezeka tangu wakati huo, huku kukiwepo uvamizi wa mara kwa mara wa jeshi la Israeli, ghasia zinazofanywa na walowezi wa Kiyahudi na mashambulizi ya mitaani yanayofanywa na Wapalestina dhidi ya Waisraeli. -Reuters #israel #wapalestina #shambulizi #vifo #Nuseirat #gaza #hamas #mateka #voa #voaswahili #mtoto #ukingowamagharibi