Mkulima: Ukosefu wa mitaji unaendelea kuwa kikwazo kwa baadhi ya wakulima

  • | VOA Swahili
    61 views
    Abdallah Mohamedi, mkulima wa miche ya karafuu kutoka mkoani Morogoro, anasema changamoto za ukosefu wa mitaji zinaendelea kuwa kikwazo kwa baadhi ya wakulima wanaotaka kupanua shughuli zao za kilimo. Amewahimiza vijana kujikita katika kilimo kama njia ya kujikwamua kiuchumi. Mohamedi ameeleza kuwa wakulima wengi wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kununua miche ya karafuu, hali inayozorotesha jitihada za kuongeza uzalishaji wa zao hilo muhimu. Ili kuwasaidia wakulima, Mohamedi huuza mche mmoja wa karafuu kwa bei ya shilingi 1,000, akilenga kuwawezesha wakulima kumudu gharama na kuongeza uzalishaji. Imeandaliwa na mwandishi wa VOA, Amri Ramadhani. #mkulima #morogoro #karafu #miche #wakulima #mitaji #tanzania #voa #voaswahili