Moshi mnene wafuka kutoka katika majengo wakati vita ikiendelea kati ya Israel na Hamas

  • | VOA Swahili
    196 views
    Kanda ya video iliyochukuliwa na ndege isiyokuwa na rubani kutoka kusini mwa Israel imeonyesha moshi mnene ukifuka kutoka katika majengo yaliyoharibiwa huko kaskazini mwa Gaza siku ya Alhamisi (Desemba 12), wakati vita vikiendelea kati ya Israel na Hamas. Vita vilianza baada ya watu wenye silaha wa kikundi cha Hamas kuzivamia jamii za Israel mnamo Oktoba 7, 2023, na kuua kiasi cha watu 1,200 na kuwateka takriban watu 250 na kuwapeleka katika eneo la Gaza, kwa mujibu wa hesabu za Israeli. Tangu wakati huo, jeshi la Israel limeharibu maeneo ya Gaza, na kuwaua karibu Wapalestina 45,000, na kuwakosesha makazi takriban wote milioni 2.3 na kuongezeka kwa njaa na magonjwa, kulingana na mamlaka ya afya za Palestina. Waisraeli na Wapalestina wanaonyesha juhudi mpya ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwaka mzima, kusitisha mapigano huko Gaza na kuwarejesha Israel angalau mateka 100 ambao bado wanashikiliwa na Wapalestina huko Gaza. - Reuters #israel #wapalestina #shambulizi #vifo #Nuseirat #gaza #hamas #mateka #voa #voaswahili