Mpox yazidi, huku vita vikiendelea DRC, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    7,662 views
    Mapigano kati ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda yanaendelea mashariki mwa nchi hiyo huku maafa yakiripotiwa Goma. Huku waasi wa M23 wakiendeleza hatua yao ya kuteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa DRC, vita hivi vimeacha janga la kibinadamu na pia kuathiri pakubwa mipango ya kutoa huduma za matibabu na kuwapa chanjo watu walio katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Mpox. Hospitali zimekosa dawa huku wagonjwa waliokuwa wametengwa wakitoroka kutoka vituo vya matibabu kwa hofu ya mapigano.