Msanii wa Kibera Atumia Sanaa Kuhifadhi Mazingira

  • | K24 Video
    81 views

    Katika makala ya kila Jumamosi ya Sauti ya Mazingira, leo tunaangazia jinsi sanaa inavyotumika kama chombo cha kuboresha na kuhifadhi mazingira. Msanii na shujaa wa mazingira kutoka Kibera, ambaye anatumia vipaji vyake kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. Kupitia sanaa na uhamasishaji, anabadilisha maisha ya wengi na kuleta mabadiliko chanya katika mazingira ya mtaa wake.