Mtu mmoja auawa kwa kupigwa risasi katika tukio la uvamizi la punde eneo la Samburu

  • | Citizen TV
    494 views

    Mtu mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi katika tukio la uvamizi la punde ambapo majangili wa wizi wa mifugo walivamia eneo la Pura Samburu magharibi. Uvamizi huo pia umemuacha mkazi mmoja akiuguza majeraha ya risasi, baada ya kufyatuliwa risasi na majangili waliojihami Kwa bunduki kabla kutoweka bila kuiba chochote. Mwanahabari wetu Bonface Barasa anaarifu zaidi kutoka Samburu.