Mzozo unatokota kati ya jamii ya Turkana na kaunti

  • | Citizen TV
    1,676 views

    Mzozo unatokota kati ya Jamii ya Turkana wanaoishi kwenye visima vya mafuta,kampuni ya uchimbaji mafuta Tullow na serikali ya kaunti ya Turkana. Hii ni baada ya kampuni ya Tullow kuilipa kaunti ya Turkana shilingi milioni mia mbili hamsini na nane mwezi uliopita. Hata hivyo, kaunti ya Turkana inasema kuwa pesa ilizolipwa ni deni ya ardhi iliyokodiwa katika maeneo ya Lokichar basin. Na kama anavyoarifu Cheboit Emmanuel Wakazi walioathirika na mradi wa mafuta wanadai mgao wa fedha hizo.