Nairobi City Thunder yafuzu ligi ya bara Afrika BAL

  • | Citizen TV
    184 views

    Timu ya Nairobi City Thunder ya Kenya hatimaye imefuzu kwa ligi kuu ya mpira wa kikapu barani Afrika BAL, baada ya kuipiku City Oilers ya Uganda katika mechi ya nusu fainali liyochezwa jana katika ukumbi wa Kasarani. Thunder ambayo imeandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza kutoka Kenya kufuzu kwa mashindano hayo, itachuana na Kriol Stars hii leo katika fainali.