Ndovu aliyehepa msituni amvyoga na kumuua mwalimu Kericho

  • | Citizen TV
    2,508 views

    Familia moja katika kijiji cha Miti Tatu eneo bunge la Kipkelion mashariki inaomboleza kifo cha jamaa yao aliyeuawa na ndovu. David Bii ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi ya Dr. Koech anadaiwa alikuwa akiwapiga picha ndovu wawili ambao walikuwa wametoka katika msitu wa Soget na kuingia katika mashamba ya wananchi. Ndovu hao wanasemekana kumgeukia na mmoja alimvyoga hadi kumuua mwalimu huyo huku mtu wa pili aliyekuwa katika eneo la tukio akijeruhiwa. Moses Mutai alipelekwa katika hospitali ya Londiani kwa matiabu. Wakaazi wanataka maafIsa wa KWS kuhakikisha ndovu hawatoki msituni na kuvamia wananchi pamoja na mimea yao. Wakati huo huo, jamaa wa mwalimu aliyeuawa wanataka walipwe fidia kufuatia mauaji yake.