Operesheni ndobo kukomesha ujambazi na wahalifu Kinshasa.

  • | BBC Swahili
    972 views
    Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, zaidi ya vijana 2,500 wahalifu maarufu kama ‘kuluna’ wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na wengine kufungwa gerezani katika muda wa mwezi mmoja uliopita. Haya ni matokeo ya operesheni ndobo, ambayo ina maana ndoano, iliyozinduliwa na serikali ili kukomesha ujambazi uliotekelezwa na wahalifu katika mji mkuu Kinshasa. Wengi wa wahalifu hao wana umri wa kati ya miaka kumi na tano hadi arobaini, na baadhi yao wamepewa hukumu ya kifo. #bbcswahili #drc #opereshenindobo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw