Pendekezo la kugawanya eneo bunge la Ruiru lashika kasi

  • | KBC Video
    21 views

    Shinikizo la kuligawanya eneobunge la Ruiru katika kaunti ya Kiambu limeshika kasi, gavana wa kaunti hiyo Kimani Wamatangi akiunga mkono hatua hiyo akisema idadi ya wakazi katika eneo hilo inaongezeka kwa kasi na kwa sasa imezidi watu elfu-700.Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji taa za barabara zinazotumia kawi ya jua katika wadi za Kahawa Sukari, Kahawa Wendani, Kiuu na Mwihoko gavana wa Wamatangi alisisitiza kuwa idadi kubwa ya wakazi wa eneo la Ruiru inahitaji upanuzi wa muundo msingi. Alisema kuwa licha ya eneobunge hilo kuwa na idadi kubwa ya watu na uwezo wake wa kiuchumu, halijakuwa likipokea raslimali za kutosha kukidhi idadi ya wakazi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive