Polisi Samburu wameanzisha operesheni ya usalama kusaka wavamizi walioiba mifugo

  • | Citizen TV
    137 views

    Vikosi vya usalama katika kaunti ya Samburu,vimeanzisha oparesheni ya kuwasaka wezi wa mifugo, waliovamia boma la Mkuu wa ukusanyaji wa madeni katika hazina ya kitaifa Haron Lesirma katika uvamizi wa leo. Idadi ya Mifugo walioibwa bado haijabainika. Wavamizi hao waliojihami Kwa bunduki wanaaminika kuvamia boma hilo mapema Leo na kuanza kufiatua risasi.