Raila akosoa ubomozi wa nyumba Kakamega

  • | KBC Video
    39 views

    Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga amekosoa ubomozi wa nyumba zilizojengwa kwenye ardhi ya serikali katika eneo la Milimani, kaunti ya Kakamega ili kutoa fursa ya ujenzi wa nyunba za gharama nafuu. Raila anadai mradi huo umeghubikwa na usiri mkubwa kwani hakukuwa na vikao vya ushirikishi wa umma kabla ya uzinduzi wake na hivyo unapaswa kusitishwa kwa kuzingatia uamuzi wa mahakama uliosema kwamba ushuru wa nyumba unakiuka katoiba. Odinga anasisitza kwamba mapendekezo mengi ya ripoti ya kamati ya kitaifa ya mashauriano yanaweza kuafikia tu kupitia kura ya maamuzi, msimamo unaopingwa vikali na mrengo wa Kenya Kwanza.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News