Rais atetea ziara yake Mlima Kenya

  • | KBC Video
    1,924 views

    Rais William Ruto amemtetea Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, kwa kuhudhuria baadhi ya mikutano yake ya hadhara wakati wa ziara yake katika eneo la Mlima Kenya. Akizungumza katike eneo la Chuka, kaunti ya Tharaka Nithi alipokuwa akizindua nyumba 60 zilizojengwa na serikali ya kitaifa kwa huduma ya kitaifa ya polisi, Rais alisema Kanja, kama Mkenya mwingine yeyote, ana kila haki ya kuhudhuria mkutano huo, ambao ulikuwa shughuli ya umma. Ruto pia aliwakashifu wakosoaji wake akisema hakuwa anafanya kampeni bali anazuru eneo hilo kukadiria mipango ya serikali na kutangamana na Wakenya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive