Rais Putin atakubali kusitisha vita Ukraine?

  • | BBC Swahili
    957 views
    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kumekuwa na majadiliano mazuri na yenye tija kati ya Urusi na Marekani kuhusu vita nchini Ukraine. Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amesema amemuomba rais wa Urusi Vladimir Putin kuonea huruma maisha ya watu na kuongeza kwamba iwapo vita vitaendelea vitasababisha mauaji ya kutisha kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.