Rais Ruto ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Namibia

  • | KBC Video
    266 views

    Rais William Ruto aliungana na wakuu wengine wa nchi na serikali katika kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah. Nandi-Ndaitwah ambaye wakati mmoja alikuwa naibu wa rais alipata asilimia 58 ya kura na kushinda uchaguzi ulioandaliwa nchini humo mwezi Novemba mwaka jana. Rais Ruto amesema Kenya inatazamia kufanya kazi kwa karibu na Namibia ili kuimarisha zaidi uhusiano wa mataifa haya mawili kwa manufaa ya raia wake.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News