Rais Ruto azuru mitaa kadha Nairobi, atetea mkataba baina yake na Raila

  • | KBC Video
    2,202 views

    Rais William Ruto ametetea ushirikiano wa kisiasa baina yake na kiongozi wa ODM Raila Odinga akisema unalenga kuleta umoja wa taifa hili. Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika eneo la Kamukunji kaunti ya Nairobi, kiongozi wa taifa vile vile alipuuzilia mbali madai kwamba makubaliano baina yake na kiongozi wa chama cha ODM, ni ya kugawana mamlaka kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Rais Ruto badala yake alisema mkataba huo uliotiwa saini katika jumba la mikutano ya kimataifa KICC unanuia kuleta ukuaji wa uchumi pamoja na maendeleo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News