Rais Trump ampa rasmi kijana heshima ya nafasi ya Usalama wa Rais

  • | VOA Swahili
    2,770 views
    Katika hotuba yake kwa Bunge, Rais wa Marekani Donald Trump alizungumzia kuongezeka kwa kiwango cha ugonjwa wa saratani na mtindio wa akili kwa watoto. Alimtambulisha D.J., kijana wa miaka 13 anayepambana na saratani ya ubongo, ambapo madaktari wake wanaamini hali yake inaweza kuwa imesababishwa na kemikali. Trump pia aligusia ongezeko la kesi za mtindio wa akili, akisema miongo michache iliyopita kila mtoto 1 kati ya 10,000 waligunduliwa wana maradhi ya mtindio wa akili, idadi ambayo hivi sasa imeongezeka na kuwa mtoto 1 kati ya 36. “Kuna kitu kimekwenda kombo,” alisema Trump, akisisitiza kuwa kufahamu chanzo kinacho sababisha na kubadili mwelekeo huu ni kipaumbele kwa serikali yake. #POTUSAddress #trump #congress #voa