Rais wa Marekani na viongozi wengine watembelea bandari ya Lobito Angola

  • | VOA Swahili
    2,339 views
    Biden akiwa ameandamana na mwenyeji wake Rais João Lourenço, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema na Makamu Rais wa Tanzania Philip Mpango akitembelea mradi wa ujenzi wa reli ya Lobito, ambapo Marekani na washirika wake wakuu wanaufadhili. Reli hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 13,000 kutoka Zambia hadi Angola kupitia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Viongozi hao vile vile wamekutana na wawakilishi wa makampuni yatakayofaidika na mradi huo ikiwemo ya mawasiliano inayoimarisha huduma zake katika eneo hilo, kampuni ya uzalishaji chakula na kampuni ya Pennyslvania inayotengeneza vyuma vya kujenga madaraja, yenye mkataba wa kuwasilisha vifaa vyake nchini Angola. #biden #us #angola #luanda #voa #rais #marekani #reli #lobito #pennyslvania #voa #voaswahili