Serikali yazindua mpango wa ‘Shirika” utakaotangamanisha wakimbizi na jamii

  • | KBC Video
    137 views

    Rais William Ruto ametoa wito wa kuwepo kwa suluhu za kudumu katika kukabiliana na idadi inayoendelea kuongezeka ya watu wanaotafuta hifadhi katika kanda hii hasa nchini Kenya. Akiongea katika ikulu ya Nairobi wakati wa uzinduzi wa mpango wa kushughulikia wakimbizi kwa jina Shirika, Ruto alisema licha ya kwamba Kenya inaendelea kuwakubali wakimbizi, kuna haja ya kuweka mikakati ya kuhakikisha wakimbizi wanajihisi nyumbani pamoja na kuhakikisha wanatangamana na jamii. Rais alitumia fursa hiyo kutoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za dharura kukomesha vita katika kanda hii, ili kupunguza idadi ya wakimbizi wanaotafuta hifadhi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive