Shambulizi la anga lililofanywa na Israel lauwa Wapalestina 7, na wengine kujeruhiwa

  • | VOA Swahili
    132 views
    Wapalestina wasiopungua saba wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatano (Desemba 11) kufuatia shambulizi la anga lililofanywa na Israel kwenye nyumba iliyoko katika kambi ya Nuseirat katikati ya Gaza, wafanyakazi wa afya wameiambia Reuters. Watu walionekana wamekaa chini, wakilia na kuomboleza vifo vya wapendwa wao huku miili ikiwa sakafuni imefunikwa na mablanketi na mifuko ya kuhifadhi miili. Wanaume na wanawake walikuwa wakifanya sala ya mazishi kwenye miili hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa. Israel na Hamas wamekuwa katika vita tangu wapiganaji wanaongozwa na Hamas walipoishambulia Israel Oktoba 7, 2023, na kuua watu 1,200 na kuwateka zaidi ya watu 250, kulingana na hesabu ya Israel. Shambulizi hilo lilichochea kampeni ya jeshi la Israeli dhidi ya Hamas huko Gaza, ambayo imeuwa zaidi ya Wapalestina 44,800, mamlaka za afya Gaza zimesema. - Reuters #israel #wapalestina #shambulizi #vifo #Nuseirat #gaza #hamas #mateka #voa #voaswahili