- 3,404 viewsDuration: 2:20Shule ya upili ya wasichana ya st. George’s jijini nairobi imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuvunja lango na kuandamana usiku wa kuamkia leo. Wanafunzi hao walikuwa wakilalamikia madai ya kupigwa na kujeruhiwa kwa mwanafunzi mwenzao na mwalimu mmoja. Wanafunzi hao wanasema matukio kama hayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara lakini yanapuuzwa na shule hiyo. Willy lusige na taarifa hiyo.