Taswira ya taifa mchakato wa kukusanya maoni kuhusu kuondolewa kwa Gachagua ikiingia siku ya pili

  • | Citizen TV
    768 views

    Saa chache baada ya Mahakama kuu ya Kerugoya kuamuru kwamba mchakato wa kukusanya maoni kuhusu mswada wa kumuondoa naibu wa Rais Rigathi Gachagua uendelee katika maeneo bunge yote kote nchini, wakenya walifika walikohitajika kutoa maoni yao. Hata hivyo baadhi ya maeneo yalishuhudia idadi ndogo ya wanachi kwa shughuli hiyo. Chrispine Otieno sasa anatupa taswira ya jinsi hali ilivyokuwa katika sehemu mbalimbali.