Timu ya FactSpace West Africa
Kwaku Asante hayuko peke yake katika vita hivi. Rabiu Alhassan ni mwandishi wa habari anayefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Yeye ndiye kiongozi wa timu ya FactSpace West Africa, shirika la kuhakiki ukweli linalofanya kazi kukabiliana na habari potofu kadhalika propaganda kote Afrika Magharibi.
GhanaFact ni sehemu ya shirika hilo.
Alhassan anasema kwake, kupambana na habari potofu ni zaidi ya kazi. Anajua madhara ya habari mbaya kwa watu wa kawaida, mataifa na kanda nzima ya Afrika Magharibi.
Vyumba vya Habari Kuunda Madawati Kuhakiki Habari
Rabiu Alhassan, kiongozi wa timu ya Fact Space West Africa aeleza: “Hatuko mbali sana kuwaona watu wenye nia mbaya wakifuatilia kile kinachofanyika nchini, kubaini makosa makubwa na kujaribu kutumia hilo. Sababu tunajaribu kutumia uwezo wetu mdogo kuleta matokeo mazuri kwa kusaidia vyumba vya habari katika kuunda madawati yao ya kuhakiki ukweli, kwa kuwasaidia wanahabari kuwa na ujuzi wa kutosha kutambua habari potofu na kukabiliana na kampeni za taarifa potofu.”
Alhassan na timu yake wanategemea vifaa kadhaa vya kidijitali kuwasaidia katika kazi yao. Kifaa marufu kati ya hivyo ni kutafuta baadhi ya picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Ana matumaini kwamba kuhakiki ukweli inaweza kupunguza taarifa potofu.
Vijana Wengi Mitandaoni
Rabiu Alhassan, kiongozi wa timu ya FactSpace West Africa:
“Tunaona vijana wengi zaidi mtandaoni, na kuna hamu zaidi ya wadau mbalimbali kuweza kudhibiti simulizi, kama tulivyoona kwenye vyombo vya habari vya kawaida pia mtandaoni. Kwa hivyo, kazi yetu imekuwa muhimu sana. Kuna matumaini makubwa katika siku zijazo, na tuna imani kwamba tutachangia kwa uwezo wetu mdogo kukabiliana na matatizo ya habari, sio tu nchini Ghana bali katika bara zima.”
Alhassan sasa anawashauri vijana wanaochunguza ukweli kujiunga na timu yake.
Timu ya FactSpace West Africa
Gifty Tracy Aminu, kutoka timu ya FactSpace West Africa: “Nimefurahishwa na ukweli kwamba ninaweza kuwaambia wananchi zaidi ya kile ambacho mtu amesema au zaidi ya kile kilichoripotiwa, nimeweza kuchunguza kwa undani kujua kwamba jambo hilo ni ukweli au la.”
#ghana #factcheck #factchecking #voa #uchunguzi #uhakiki #habaripotofu #accra #waandishi #rabiualhassan #factspacewestafrica #factcheckghana #KwakuAsante