Uchunguzi wa mauaji ya mwanaharakati Rex Masai wasitishwa

  • | K24 Video
    242 views

    Uchunguzi wa mauaji ya mwanaharakati Rex Masai umesitishwa baada ya kufichuliwa kuwa shahidi muhimu wa serikali, afisa wa polisi, hakuwa ametoa stakabadhi husika kwa pande zingine alizotarajia kuzitegemea wakati wa ushahidi wake. Fredrick Ole Tepes, aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha central alitarajiwa kujieleza hata hivyo, mahakama ilisikiliza kuwa upande wa mashtaka haukuwa umewasilisha nakala za ushahidi wake kwa mawakili wa pande zote mbili..