Usaili wa mwenyekiti na naibu wa IEBC waanza Nairobi

  • | KBC Video
    289 views

    Suala la uadilifu na mtu anayefaa kushikilia afisi ya umma lilitawala mwanzoni mwa shughuli ya usaili wa wawaniaji walioorodheshwa kuwania nafasi ya uenyekiti wa tume ya uchaguzi, IEBC. Anne Amadi alimulikwa kuhusiana na kashfa ya dhahabu ya mwaka 2023 ambayo alipuuza akisema lilikuwa ni jaribio la mahasimu la kutoa doa uadilifu wake. Naye aliyekuwa jaji wa mahakama ya Afrika mashariki Charles Nyachae alikuwa na wakati mgumu kujibu madai ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake pamoja na kashfa kuhusiana na waraka uliowasilishwa na vuguvu la Bunge la Mwananchi. Abdiaziz Hashim ana mengi kuhusu siku ya kwanza ya mahojiano ambapo wawaniaji wanne kati ya 11 walisailiwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News